Image
Image

EXCLUSIVE: TENGA ATANGAZA RASMI KIKOSI CHA STARS


Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) Leordger chila Tenga ametangaza kikosi cha Taifa stars chenye uwezo wa kuweza kukabiliana na mikiki mikiki katika mashindano yoyote yale kutokana na uimara wake.

Mapema leo  Tenga wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya stars kwenye Hotel ya Tansoma  jijini dar es salaam amesema kuwa kiwango walicho onyesha wachezaji hao kwenye mechi zilizokuwa zimepita za mchujo  kama ya Morocco na Ivory  imethibitisha tosha kiwango cha timu hiyo.

"Kiwango mlichoonyesha katika mechi hizo kila mtanzania anayewafuatilia amekiona, hivyo hatuna shaka kuwa mtatuwakilisha vizuri kwenye mechi ya kesho dhidi ya uganda," amesema rais tenga na kuwataka kupigana kwa ajili ya tanzania.

Tenga amesema TFF, mdhamini kilimanjaro premium lager, kamati ya ushindi na watanzania kwa ujumla wanawaunga mkono kwani wamekuwa wakiboresha kiwango chao kila wanavyozidi kucheza mechi tangu wake chini ya kocha kim poulsen, mei mwaka jana.

Taifa stars inayodhaminiwa na kilimanjaro premium lager kesho (julai 13 mwaka huu) saa 9 kamili alasiri uwanja wa taifa, dar es salaam itacheza na uganda (the cranes) katika mechi ya kwanza ya raundi ya mwisho kuwania tiketi ya kucheza fainali za chan zitakazofanyika mwakani nchini afrika kusini.

Wakati huo huo,  tenga ameahidi kumpatia tiketi ya kwenda uganda kwenye mechi ya marudiano mshabiki wiseman mwakyusa luvanda anayetembea kwa miguu kutoka mbeya kuja dar es salaam kushuhudia mechi ya kesho.

"Kama ni kweli anakuja kwa kutembea, huyu ameonyesha kiwango kikubwa cha uzalendo kwa timu ya taifa, nitampatia tiketi ya kwenda kampala kuishangilia taifa stars kwenye mechi ya marudiano," amesema rais tenga.

Katika hatua nyimngine makocha wa timu hizo kim poulsen wa taifa stars na sredojvic micho wa the cranes wamesema mechi ya kesho itakuwa ngumu kwa vile kila mmoja amejiandaa kuhakikisha anafanya vizuri.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo, makocha wote waliezea ubora wa wapinzani wao, lakini wakasisitiza kuwa wanaingia uwanjani kuhakikisha wanashinda ili kujiweka katika mazingira mazuri kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa kampala wiki mbili zijazo.

kim alisema uganda ndiyo inayoongoza kwa ubora wa viwango vya fifa katika ukanda huu wa afrika mashariki na kati, hivyo ni changamoto kwao ingawa wachezaji wake tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.

Kwa upande wake micho aliyefuatana na nahodha wake hassan wasswa alisema taifa stars imekuwa ikifanya vizuri tangu iwe chini ya kim, na itakuwa na wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kinachocheza mechi za mchujo za kombe la dunia wakati kwa upande wake atakuwa na wachezaji wawili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment