Jakaya Kikwete
Tanzania
imekabidhi rasmi uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC-Troika)
kwa Namibia, huku ikielezea mafanikio yaliyopatikana katika kushughulikia
changamoto za kisiasa na usalama kwenye mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, Zimbabwe, Madagascar.
Mwenyekiti wa
SADC - Troika aliyemaliza muda wake Rais Jakaya Kikwete, anayemaliza muda wake
wa uongozi akizungumza nchini Malawi katika mkutano wa 33 wa wakuu wa Jumuiya
ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC, ametoa taarifa ya utendaji
katika kushughulikia mizozo ya kiasiasa miongoni mwa nchi wanachama ambapo
ameitaka Namibia na nchi wanachama wa SADC kusimamia mpango wa amani na maagizo
ya SADC, Umoja wa Afrika, umoja wa Mataifa katika kutatua mzozo wa uongozi
Madagascar ili kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu kwa lengo la kumaliza mzozo
wa kisiasa nchini humo.
Rais
Hifikepunye Pohamba, wa Jamhuri ya Namibia amepokea Uenyekiti wa Asasi ya
Siasa, Ulinzi na Usalama ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za
kusini mwa Afrika SADC-Troika kwa
kipindi cha mwaak mmoja .


0 comments:
Post a Comment