Image
Image

WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MOROGORO BAADA YA KUPATIKANA NA MENO YATEMBO KILO 40


                                         Faustine Shilogile.


Na.Jimmy Mengele,Morogoro.

 Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu wawili pamoja na gari walilokuwa wakisafiria baada ya kupatikana na meno ya tembo kilo arobaini na tano nukta tano yenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni thelathini na tisa na laki tatu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile amewaambia waandishi wa habari mjini Morogoro kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori kutoka hifadhi ya taifa ya Udzungwa katika eneo Mzombe darajani kata ya Kidodi  barabara ya Ifakara Mikumi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Amesema watuhumiwa hao walikamtwa wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 199 AQP  Mitsubish Fuso lori ambalo lilikuwa limepakia magunia ya mchele ambapo katika upekuzi, askari walifanikiwa kukuta meno hayo yakiwa kwenye mfuko wa sandarusi(Sulphate) .
Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Udzungwa  Nitalis Uruka, pamoja na mkuu wa kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya mashariki, wizara ya maliasili na utalii Faustine Masalu wamezungumzia ujangili huo, pamoja na kuwawasisitizia wananchi kukabiliana na vitendo hivyo vinavyoshika kasi nchini vinavyoathiri maliasili ya taifa ambayo inapaswa kulindwa kwa maslahi ya kizazi  vya sasa na vijavyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment