Angela Kairuki.
Zahanati
pamoja na vituo vya afya vitano katika wilaya ya Kinondoni jijini dar es Salaam
vimepokea msaada wa vitanda 20 pamoja na magodoro wenye thamani ya jumla ya
shilingi milioni 50 kwa ajili ya akina mama wanaojifungua.
Akikabidhi
msaada huo katika moja ya zahanati iliyoko Kimara jijini dar es Salaam Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki amesema vifaa hivyo ni miongoni mwa
mahitaji muhimu yanayotokana na ongezeko la wagonjwa pamoja na kuzijengea uwezo
hospitali hizo ili kupunguza msongamano katika hospitali za mikoa.
Aidha kwa upande wake mganga Mkuu Mfawidhi katika zahanati ya kimara Dk.Alphonsina Mbinga amesema zahanati hiyo ambayo inahudumia kati ya wagonjwa 500-hadi 600 kwa siku inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa watumishi pamoja na gari la wagonjwa .



0 comments:
Post a Comment