Augustine
Mgendi, Mara.
Serikali
kupitia Wizara ya Nishati na Madini nchini imekamilisha upimaji wa Viwanja 35
katika eneo la Rwabasi lililopo Buhemba wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa ajili
ya wachimbaji wadogo wa Dhahabu.
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi Angelina Mabula Kufuatia kupatikana
kwa Mwekezaji kutoka nchini Australia
ambapo amesema kukamilika kwa zoezi hilo ni kutokana na kauli ya Waziri
wa Nishati na Madini Prof Sospeter
Muhongo katika hotuba yake ya Bajeti kwa
mwaka 2013/2014 iliyowahakikishia
wachimbaji wadogo katika kata za Buhemba na Mirwa kutengewa eneo la uchimbaji
wa Madini ya Dhahabu.
Amesema zoezi
hilo limekuwa shirikishi kwa wachimbaji wa Maeneo hayo na hivyo kuwataka kuunda
vikundi ili kupata Leseni zitakazowezesha kufanya shughuli za Uchimbaji katika
Maeneo hayo.
Aidha Mkuu
huyo wa Wilaya amesema mbali na wachimbaji hao Wadogo kutengewa maeneo
Uchimbaji lakini pia Wananchi wa eneo la Buhemba watanufaika na kuwepo kwa
uwekezaji huo huku kamishina Msaidizi wa Madini kanda ya Ziwa akisema kuwa
ofisi yake itafanya Mafunzo kwa wachimbaji wadogo mkoani Mara kuhusu utunzaji
wa Mazingira,kujua sheria za Madini na ulipuaji wa miamba katika njia salama.
Serikali
kupitia Wizara ya Nishati na Madini imempata Mwekezaji Kampuni Manjaro Resource
kutoka nchini Australia ambapo itashirikiana na Kampuni ya STAMICO kufanya Shughuli za Uchimbaji wa Madini
katika Mgodi wa Buhemba uliopo wilaya ya
Butiama Mkoani Mara.



0 comments:
Post a Comment