Rachel Balama na Anneth
Kagenda.
SIKU chache baada ya Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini kudai jeraha alilonalo katika bega la
kulia limetokana na risasi aliyopigwa na polisi mkoani Morogoro, baadhi ya
Waislamu nchini wametoa tamko la kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu mara moja.
Msimamo huo umetolewa Dar es
Salaam jana katika kongamano la Waislamu ambalo lilifanyika katika Uwanja
wa MwembeYanga.Akizungumza katika
kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na mamia ya waumini wa dini hiyo, mmoja wa
viongozi wa jumuiya hiyo Shekhe Kondo Juma Bungo, alisema
Waislamu wanatoa muda kwa Dkt. Nchimbi kujiondoa katika nafasi hiyo.
Alisema, mbali na Dkt. Nchimbi,
walisema Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile, anapaswa
kukamatwa na kufikishwa mahakamani wakidai ndiye mhusika mkuu wa
kupanga mikakati ya kumdhuru Shekhe Ponda.
“Askari aliyempiga
risasi Shekhe Ponda na Kamanda ambaye alisimamia suala zima
la uvamizi kwa kiongozi wetu, wote wanapaswa kuwajibishwa.
tunataka iundwe tume huru ya
uchunguzi badala ya timu
iliyoundwa na
polisi,” alisema.
Al i o n g e z a k uwa , kama
maazimio hayo yatapuuzwa na
wahusika pamoja na Serikali
kushindwa kuchukua hatua stahiki, itakuwa mwanzo na mwisho wa historia ya
Tanzania.
“Kitakachotokea baada ya hapo,
Serikali itaona mwanzo tu lakini haitajua mwisho wake...Waislamu nchi
nzima
watafanyamaandamano, polisi
wanategemea kupandishwa vyeo au kupewa posho nyingi pale yanapotokea
matatizo ya
Waislamu. “Kwa sasa hali
inavyoonesha watapandishwa vyeo kwa uchungu kwani Waislamu
hatutakubali,” alisema Shekhe
Bungo na kusisitiza kuwa,
Shekhe Ponda ana thamani kubwa sana kwa Waislamu.
Shekhe Bungo alilihadharisha
Jeshi la Polisi kuacha kuwatisha Waislamu na kuongeza kuwa, Serikali isije
kuwalaumu kwa kitakachotokea kama madai yao hayatatekelezwa.
Aliwataka Waislamu popote walipo,
kutoa adhabu palevion gozi au wanachama wa Cha maChaMapinduzi
(CCM),wanapoingia misikitinina kufanya kampeni za kuomba wachaguliwe
katika uchaguzi ujao.
Tamko la CUF
Katika hatua nyingine,Chama cha
Wananchi (CUF), kimelitaka Jeshi la Polisi nchini,limuachie Shekhe Ponda
aweze kuendelea na matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (M OI)
.
Chama hicho kimesema kitendo
alichofanyiwa Shekhe Ponda cha kuondolewa MOI wakati hali yake kiafya
haijatengemaa, sichakibinadamu bali cha kinyama.
Mwenyekiti wa chama hicho
Taifa,Profesa Ibrahim Lipumba,
aliyasema hayo Dar esS alaam jana
wakati akizungumza na
waandishi wahabari.
"Kauli za vitisho na ubabe
unaofanywa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna
Suleiman Kova, vinachochea hasira na jazba za wananchi wengine
wakiamini kuwa, jeshi hilo lina lengo la kumuua Shekhe Ponda badala ya
polisi kujenga amani, wao wanaibomoa," alisema.
Prof. Lipumba alisema, jeshi hilo
limeshindwa kufanya kazi kwa weledi ndio sababu ya kuongezeka vitendo vya
uhalifu na tuhuma nyingi kwa baadhi ya polisi ambao wanashirikiana na
wahalifu.
"Polisi wetu wameweka
pembeni kazi yao ya kupambana na uhalifu... wanapoteza wakati mwingi na
raslimali
kumshughulikia Shekhe Ponda
hivyo nawaomba Watanzania wote tudai jeshi lenye weledi na
linalowajibika," alisema.
Alisema CUF kinaungana na
Watanzania wote kulaani vikali
kitendo alichofanyiwa Shekhe
Ponda, kumfungulia mashtaka na kumuondoa MOI alipokuwa akipatiwa matibabu
bila taarifa na kumpeleka gerezani Segerea.
Aliongeza kuwa, jeshi hilo ndio
chanzo cha wananchi kuvunja
amani ya nchi ambapo juzi
mchana, alikwenda Segerea kumuona Shekhe Ponda ambapo Mkuu wa gereza hilo
alimpa ushirikiano mzuri uliofanikisha amuone na kuzungumza naye.
" Ta y a r i S h e k h e P o
n d a amepelekewa dawa zake gerezani na amepewa huduma za tiba zinazoweza
kupatikana katika gereza hilo," alisema Prof. Lipumba na kuongeza
kuwa, taarifa alizonazo X-ray imeonesha risasi aliyopigwa imepita karibu
na mfupa ambao umepasuka.
Alisema hali ya Shekhe Ponda
inaendelea vizuri ukilinganisha
na awali baada ya
kufikishwa gerezani kwani anaweza
kutembea mwenyewe, anafahamu
kamili na waliweza kutaniana na mkuu wa gereza ambaye alimhakikishia
kupata huduma nzuri.
Prof. Lipumba aliongeza kuwa,
anazo taarifa kuwa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linataka kumhoji
daktari aliyemtibu Shekhe Ponda, siku alipopigwa risasi.
"Inasikitisha kwamba polisi
hawajapitia Taasisi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), ili iombe
kibali cha kufanya hivyo badala yake wanataka kumsulubu daktari kwa kosa
la kumtibu Shekhe Ponda jambo ambalo linashangaza," alisema.
Aliongeza kuwa, CUF inataka
Serikali iunde tume huru ambayo itaongozwa na Jaji ili kuchunguza tukio la
kupigwa risasi Shekhe Ponda, askari aliyempiga na waliompa amri ya kufanya
hivyo wafikishwe mahakamani na kumfutia kesi ya uchochezi.
Shekhe Ponda alipata mkasa huu
Agosti 10 mwaka huu mkoani Morogoro muda mchache baada ya kushiriki katika
Kongamano la Baraza la Eid.
CHANZO
http://mambomseto88.blogspot.com



0 comments:
Post a Comment