Mama na mwanae wameuawa
kikatili baada ya kukatwa mapanga na baadhi ya viungo vyao kuchomwa moto katika
tukio linalohusishwa na imani za kishirikina lililotokea mkoani Shinyanga.
Wanawake hao
vikongwe mtu na mtoto wake ni Jadi Temi (90) na mwanae Samara Mathias (70)
wakazi wa kijiji cha Ikonda wilayani Shinyanga.
Wawili hao
walishambuliwa na kuuawa juzi na watu wasiojulikana wakiwa wamekaa nje ya
nyumba yao wakiota moto na kufurahi chakula cha usiku.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Shinha Kihenya Kihenya, alisema vikongwe walishambuliwa na mapanga
sehemu mbalimbali za miili yao na kufa papo hapo huku baadhi ya viungo vya
Samara vikitupwa kwenye moto uliokuwa jirani.
Kihenya alisema tukio
hilo lilitokea Ijumaa saa 2:00 usiku katika kijiji cha Ikonda wilayani
Shinyanga, wakati wawili hao wanaoishi peke yao wakila chakula na kuota moto.
Kihenya alifafanua
kuwa mara baada ya kushambulia na kuua wauaji hao wakikata kichwa cha Samara,
kiganja cha mkono wa kushoto na mguu wa kulia na kuvitupa kwenye moto uliokuwa
jirani.
Alisema wauaji hawakuiba
chochote na kuna wasiwasi kuwa mauaji hayo yayamefanywa kutokana na ushirikina
.
Shinyanga Blog.


0 comments:
Post a Comment