Image
Image

HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM YARIDHIA UAMUZI WA KUVULIWA UANACHAMA WA CHAMA HICHO MWAKILISHI WA KIEMBE SAMAKI MANSOOR YUSUF HIMID VISIWANI ZANZIBAR.



                          Mansoor Yusuf Himid.
 Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Wilaya Mjini Magharibi Zanzibar wa kumvua uanachama wa chama hicho Mwakilishi wa Kiembe Samaki  Mansoor Yusuf Himid.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada Halmashauri Kuu ya Taifa kumaliza kikao chake, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) Bw. Nape Nnauye amesema kikao hicho kimeridhika na tuhuma zilizokuwa zinamkabili mjumbe huyo wa Baraza la uwakilishi.


Aidha, Kwa mujibu wa Katibu huyo mwenezi wa (CCM) kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa, kimewateua Bw. Romuli Rojas John, Bw. Kassim Mabrouk Mbarak na Bi. Mary Maziku, kuwa makatibu wa mikoa, ambapo watapangiwa vituo vya kazi hapo baadaye.

Kuhusu, sakata la madiwani wa (CCM) Bukoba Mjini, Bw. Nape amesema maamuzi yatatolewa baada ya viongozi wote husika kusikilizwa na Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama hicho.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment