Image
Image

JESHI LA POLISI MKOANI MOROGORO LAMTAKA SHEKH PONDA KUJITOKEZA MBELE YA JESHI HILO NA KUTHIBITISHA TAARIFA ZA KUPIGWA KWAKE NA ASKARI.


                                          Shekh Ponda.

Polisi mkoani Morogoro imemtaka Shekh Ponda Issa Ponda kujitokeza mbele ya Jeshi hilo kuthibitisha taarifa za kupigwa risasi katika tukio lililotokea baada ya kongamano lililoandaliwa na wahadhiri wa dini ya kiislamu.

Taarifa zinadai kuwa shekh Ponda alipigwa risasi begani majira ya saa 12 jioni baada ya kongamano hilo wakati akisindikizwa na wafuasi wake wa dini ya kiislamu kuelekea katika msikiti wa mungu mmoja dini moja.
                                          Shekh Ponda
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Faustin Shilogile amesema polisi wakiwa katika harakati za kumkamata Shekh Ponda kwa makosa ya uvunjifu wa masharti aliyopewa na mahakama, walifyatua risasi za baridi kuwatawanya wafuasi waliokuwa wakisukuma gari la sheikh Ponda.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments: