Hawa ni askari wa jeshi la polisi mkoani mwanza wakiwa katika harakati za kuwatawanya wafuasi wa chama cha Democrasia na maendeleo chadema kufuatia kuibuka vurugu jijini humo.
Henry Kavirndo Mwanza.
Jeshi la
polisi mkoani Mwanza leo limelazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kutaka kuandamana hadi
katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo kumshinikiza kutoa
majibu ya kutaka kumvua wadhifa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani
humo Henry Matata na Naibu wake Swila Dede.
Suala jingine
ambalo wafuasi wa chama hicho wanalihitaji ni kurejeshwa pia Madiwani watatu wa
chama hicho waliovuliwa wadhifa huo.
Jeshi hilo
limelazimika kuingilia kati maandamano hayo baada ya wafuasi wa chama hicho
kufanya maandamano yaliyoanzia kata ya nyakato mkoani Mwanza na kuhitimishwa
katika viwanja vya furahisha ambapo kwa mujibu wa duru za awali yalitarajiwa
kupokewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo ambaye hata hivyo hakuweza
kufika uwanjani hapo.
Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema wakionekana kubeba mabago kwa lengo la kudshinikiza
baada ya kutaka kuandamana hadi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo kumshinikiza kutoa majibu ya kutaka kumvua wadhifa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani humo.
Kutokana na
mkuu huyo wa mkoa kutowasili uwanjani hapo kama ilivyotarajiwa kulingana na
duru zilivyokuwa zimetanda mkoani hapa kwamba angeyapokea maandamano hayo wafuasi
wa chama hicho ambao walikuwa wamekaa uwanjani hapo kwa muda mrefu wakimsubili
mkuu huyo wa mkoa waliamua kuanzisha maandamano ya dharula ya kutaka kumfuata
ofisini kwake.
Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema wakionekana kubeba mabago kwa lengo la kudshinikiza
baada ya kutaka kuandamana hadi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo kumshinikiza kutoa majibu ya kutaka kumvua wadhifa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani humo.
Katika vurugu
hizo baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo wafanyabiashara walijikuta
wakilazimika kusitisha shughuli zao za kibiashara na wengine kuzikimbia ili
kukwepa kudhurika na moshi wa mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa
kuwatawanya wafuasi wa chadema.
Mtaa ukionekana kuwa safi kwa masaa machache baada ya askari hawa wa ffu kuwatawanya wafuasi hao.
Awali akizungumza
na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo amesema kuwa
hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa linashughulikiwa kisheria.
Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema waliwasha moto katika eneo hili, hapa askari wa kutuliza ghasia wakionekana kuondoa mawe baada ya kutuliza vurugu hizo jijini mwanza.
Wafuasi wa
chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamelazimika kufanya maandamano
hayo yaliyokuwa yakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Highnes Kiwia pamoja
na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Ezekiah Wenje baada ya uchaguzi wa viongozi hao
kupigwa kalenda tangu kikao cha kamati kuu ya Chama hicho Taifa kilipowavua
uanachama ili kusubili maamuzi ya kisheria.








0 comments:
Post a Comment