Wanajeshi 35
kutoka jeshi la ulinzi la wananchi wa TANZANIA,JWTZ,wameondoka jana kuelekea
nchini ANGOLA,kushiriki mazoezi ya kijeshi ya pamoja kwa nchi za SADC
yanayotarajiwa kufanyika nchini humo kuanzia leo na kuhusisha vikosi vya anga
pekee.
Akizungumza na
wanajeshi hao kabla hawajapanda ndege, mkuu wa vikosi makao makuu ya Jeshi,
Meja Jenerali HASSAN CHEMA, amewakumbusha wanajeshi hao kuzingatia nidhamu ya
hali ya juu kwenye ushiriki wao na kuhakikisha sifa ya majeshi ya Tanzania
katika weledi na uadilifu vinaendelea.
Amesema
mazoezi hayo yajulikanayo kama BLUE ZAMBEZI 2013 yanafanyika kwa mara ya nne
sasa, ambapo tanzania imekuwa ikishiriki mara zote likiwamo zoezi lililojulikana
kama BLUE RUVUMA ambalo limewahi kufanyika hapa nchini katika mikoa ya LINDI na
MTWARA.
Awali akisoma
taarifa kabla ya kukagua na kupitisha gwaride rasmi la askari hao, mkurugenzi
wa ufundi makao makuu ya jeshi, BRIGADIER GENERALI OMARI MATEKA, alisema
wamejiandaa kikamilifu kushiriki zoezi hilo na kuahidi kuonesha uzoefu walionao
katika kukabiliana na majanga mbalimbali.
Wanajeshi hao
kabla ya kupanda ndege ya jeshi kuelekea Angola walifanya gwaride fupi na kutoa
heshima zao kwa mgeni rasmi meja
jenerali Hassan Chema ambaye mara tu baada ya gwaride alikabidhi bendera ya
TANZANIA kwa kiongozi wa msafara huo ambae ni brigadier generali Matteka na
kisha kuwapa mkono wa kwaheri.
0 comments:
Post a Comment