Tume ya
mabadiliko ya katiba imetakiwa kuyatupilia mbali mapendekezo ya rasimu ya
mabadiliko ya katiba yatakayotolewa na Baraza la Wanafunzi wa Vyuo vikuu na
taasisi za elimu ya juu Zanzibar, baada ya kuzuiliwa kwa wajumbe kutoka vyuo
vikuu viwili visiwani humo.
Jumla ya vyuo
vikuu 11 kati ya 13 vilivyopo Zanzibar vinawakilishwa na wajumbe 106, lakini
wajumbe 47 ndio wanaoshiriki katika mchakato huo, huku wajumbe 20 wa Baraza la
katiba kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar na Chuo cha Maendeleo ya Utalii
wakitimuliwa baada ya kupinga msimamo wa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kuhusu
Muungano.
Wakizungumza
na Tambarare Halisi katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kilichopo
Beitrasi, wanafunzi waliofukuzwa wamesema endapo tume itapokea maoni hayo
itakuwa haijawatendea haki wanafunzi wa Vyuo vikuu ambao wamekosa kutoa yao
kutokana na kufukuzwa kwa wawakilishi wao.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya
juu Zanzibar, Juma Kombo Hamad amesema wajumbe wa baraza hilo wamefikia uamuzi
wa kuwafukuza kutokana na kitendo chao cha kususia kikao na kutangaza kujiondoa
katika mchakato huo.
0 comments:
Post a Comment