Image
Image

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LAFANIKIWA KUOKOA SHILINGI MILIONI 15 KATI YA 28 ZILIZOKUWA ZIMEIBWA NA MAJAMBAZI JIJINI DAR ES SALAAM





Khamis Suleiman, Dar es Salaam.




Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kuokoa shilingi millioni 15 kati ya shilingi millioni 28 zilizoporwa na majambazi wawili kwa mfanyabiashara William Mathias eneo la Buguruni malapa jijini Dar es salaam.

Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam CP Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari amesema majambazi hao wakiwa na silaha walimvamia mfanyabiashara huyo baada ya kumfuatilia na baadae kumtishia kwa silaha na kumpora fedha hizo.
Mara baada ya uporaji wananchi pamoja na waendesha bodaboda walianza kuwafukuza ambapo majambazi hao walitumia mbinu ya kurusha fedha ili watoroke lakini walidhibitiwa na polisi waliokuwapo eneo hilo.
Aidha katika kupambana na madawa ya kulevya jeshi hilo limefanikiwa kukamata shehena ya madawa ya kulevya aina ya bangi yakiwa katika mabegi makubwa kumi, na mapipa matano pamoja na kuwashikilia watuhumiwa 231, ambapo pia imekamata mtandao wa wezi wa vioo vya magari, na vioo vya magari zaidi ya elfu moja.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi linawashikilia wafanyakazi wawili wa shirika la umeme tanesco kwa wizi wa Transfoma mbili kutoka katika ghala la tanesco lililopo kinondoni jijini dsm.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment