Shekh Ponda Issa Ponda aliyevaa shati nyekundi akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili dhidi yake.
Jimmy Mengele Morogoro.
Katibu wa
jumuiya na taasisi za kiislamu nchini Shekh Ponda Issa Ponda amesafirishwa kwa
na helkopta ya jeshi la polisi katika
mahakama ya hakimu mkazi mkoani Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili
ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini
na kushawishi kutenda kosa kinyume na mashariti ya kifungo cha nje
alichohukumiwa na mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu.
Hili ni gari la polisi ambalo lilikuwa linahakikisha kwamba ulinzi unaimarika katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani morogoro alikokuwa Sheikh ponda issa ponda akisomewa mashitaka matatu yaliyokuwa yakimkabili dhidi yake leo hii.
Shehe Ponda
akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi amewasili mkoani Morogoro
akitokea jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusomewa mashitaka katika mahakama
ya hakimu mkazi mkoani Morogoro majira ya saa tano asubuhi kwa helkopta ya
jeshi la polisi.
Hii ni helkopta ya jeshi la polisi iliyokuwa imembeba katibu wa jumuiya na taasisi za kiislamu nchini sheikh ponda issa ponda kwa kusomewa mashitaka yanayo mkabili katika mahakama ya Hakimu mkazi mkoani morogoro.
Akisomewa
mashitaka hayo akiwa amekaa kutokana na kudai kuwa na maumivu ya jeraha kwenye
bega, wakili mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard Kongola amedai kuwa
Shekh ponda anatuhumiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira
ya jioni katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege Manispaa ya
Morogoro.
Shekh Ponda Issa Ponda aliyevaa shati nyekundi akiwa katika Ndege kwenye mahakama ya hakimu mkazi mkoani Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili dhidi yake huku jeshi la polisi likionekana imara kweli kweli.
Katika
shitaka la kwanza la Shekhe Ponda anadaiwa kutotii amri halali ambapo shitaka
la pili anadaiwa kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa
maneno ambayo yamenukuliwa yakisema ìSerikali iliamua kupeleka jeshi Mtwara
kushughulikia suala la vurugu zilizotokana na gesi kwa kuwaua na kuwatesa
wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa Mtwara ni waislamu kitendo ambacho
ni kosa la jinai kifungu 129.
Shitaka la
tatu linalomkabili Shekh Ponda ni kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa
kutoa maneno ya ushawishi kwa waislam kutokubali uundwaji wa kamati za ulinzi
na usalama za misikiti akidai zinaundwa na BAKWATA ambao ni vibaraka wa CCM na
serikali.
Baada ya
kusomewa mashitaka hayo Sheikh Ponda anayetetewa na mawakili Barthoromew Tarimo
na Ignas Punge, amekana mashitaka yote na hivyo upande wa mashitaka kupinga
dhamana kwa madai kuwa Shekh Ponda anatumikia kifungo cha nje na kwamba
hakutakiwa kufanya kosa.
Shekh Ponda Issa Ponda aliyevaa shati nyekundi akiwa akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili dhidi yake.
Aidha upande
huo wa mashitaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo
mshitakiwa atarudishwa mahakamani Agosti 28 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa
maelezo ya awali ya mashitaka yanayomkabili na kwa sasa amerejeshwa rumande.
0 comments:
Post a Comment