Image
Image

BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA KUJADILI MAENDELEO YA MILENIUM KWA WATU WENYE ULEMAVU.



 Dkt.John Ashe, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa


Joshua Mmali Massoi.
katika kuelekea kuanza kwa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo kesho Jumanne,leo baraza hilo limekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuhusu kufikia malengo ya maendeleo ya milenia na malengo mengine ya kimataifa kuhusu watu wenye ulemavu.  

Kikao hicho cha ngazi ya juu kikijumuisha washiriki kutoka nchi mbali mbali ikiwemo watu wenye ulemavu kimejikita zaidi katika azimio lenye lengo la kuweka maendeleo yanayojumuisha makundi yote hususan kundi hilo muhimu katika ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. 

Rais wa mkutano wa 68 wa Baraza Kuu Dkt. John William Ashe amesema azimio hilo lina vipengee muhimu vya kuhakikisha walemavu hawaachwi nyuma iwapo jamii inataka kupata maendeleo endelevu.

Jambo moja muhimu na la haraka ni kuhakikisha majengo yote, vifaa na maeneo ya umma yanaundwa mahsusi kwa ajili ya kutumiwa na kufikika kirahisi na watu wenye ulemavu na kuwa teknolojia mpya zinapatikana ili kuboresha hali yao ya maisha na kuwapa uwezo wa kuendeleza shughuli zao za kazi na kujumuika pamoja na jamii katika hali ya kawaida."

Mwanamziki mashuhuri wa Kimarekani, Stevie Wonder, mwenye ulamavu wa macho, na ambaye pia ni balozi mwema wa amani wa Umoja wa Mataifa, amezitaka serikali ziwekeze zaidi katika teknolojia ya kuwasaidia watu wenye ulemavu.

"Ni lazima tuifanye teknoljia hii kupatikana kwa watu wenye ulemavu kote duniani. 

Ningependa kuwaomba nyotte na nchi zote, hata kama ni kuwekeza fedha za serikali katika teknolojia hii- ila sio tu ushuru upunguzwe, lakini pia  kila mtu mwenye ulemavu aweze kujitegemea na kujisikia huru."

Kwa upande wa mama huyu  Gertrude Oforowa kutoka Ghana, amekuwa na ujumbe huu kuhusu malengo ya maendeleo na watu wenye ulemavu.

"Ulemavu ni lazima uwe sehemu ya maendeleo jumuishi, kama suala muhimu katika kila uwanja, na malengo mahsusi, na njia ya kufuatilia uendelezaji na ujumuishaji ili tuwe na ubora wa maendeleo kati ya sasa na 2015, na pia baada ya 2015."
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment