Image
Image

MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA IMERIPOTI KUWA MAENDELEO MAKUBWA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA VVU.




Kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kimepungua kwa theluthi moja katika muongo mmoja uliopita kutokana na kuongezeka kwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya matibabu na kupatikana kwa dawa zenye ufanisi. 

Ripoti iliyotolewa na shirika la kimataifa ya kupambana na Ukimwi UNAIDS inasema mwaka 2012 kulikuwa na maambukizi mapya milioni 2.3, idadi ambayo imepungua kwa asilimia 33 kuliko mwaka 2011. 

Tathmini hiyo pia inasema hadi kufikia mwaka 2012 watu milioni 9.7 katika nchi zenye mapato ya chini na ya kati waliweza kupata dawa za ARV, likiwa ni ongezeko la asilimia 20 kwa mwaka mmoja. 

Hata hivyo tathmini hiyo inasema kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia, udhaifu kwenye sheria na ubaguzi vinaendelea kukwamisha juhudi za mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment