Image
Image

UGANDA YAIMARISHA USALAMA KWENYE MIPAKA YAKE.




Msemaji wa Jeshi la Uganda amesema ulinzi na usalama kwenye mipaka nchi hiyo umeimarishwa. 

Uganda kama ilivyokuwa Kenya ambayo imetuma vikosi vyake nchini Somalia kupambana na wanamgambo wa al Shabab, imeingiwa na wasiwasi wa uwezekano wa kutokea shambulio kama hilo nchini humo. 

Kundi la al Shabab lilitangaza kuhusika na shambulio hilo ikiwa ni jibu kwa serikali ya Kenya ambayo ilituma wanajeshi wake nchini Somalia.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la al Shabab liliwahi kutekeleza shambulio la kigaidi na kuwaua watu 77 katika jiji la Kampala waliokuwa wakiangalia fainali za soka za kombe la dunia mwaka 2010, zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

Paddy Ankunda ameongeza kuwa, jeshi la Uganda limeimarisha ulinzi na usalama kwenye mipaka ya nchi hiyo kufuatia shambulio la wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab linalofungamana na mtandao wa al Qaeda ambao wamewaua, kuwajeruhi na kuwateka nyara watu kadhaa  waliokuwa kwenye jumba la kibiashara la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment