Image
Image

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya China na Afrika yatafuta njia za kuimarisha ushirikiano katika kuboresha maisha ya watu




Kongamano la kuhimiza maendeleo ya maisha ya watu wa China na Afrika lilifanyika Beijing. 

Wajumbe wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya China na Afrika walihudhuria mkutano huo. 

Afrika ni moja ya kanda zinazoendelea kwa kasi zaidi duniani, na maendeleo ya kasi yanahitaji uungaji mkono wa uzoefu, teknolojia, fedha na wataalamu, ndiyo maana Afrika imekuwa soko muhimu na eneo la uwekezaji kwa China. 

Katibu wa shirikisho la China la kuhimiza mawasiliano ya kimataifa ambaye pia ni meneja mkuu wa kampuni ya kutengeneza mashine nzito cha China Bw. Lu Wenjun alisema, kuboresha miundombinu na kuinua kiwango cha maendeleo ya kilimo ni mambo muhimu kwa maendeleo ya Afrika. Akisema: 

"kampuni yetu ilishiriki kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya utoaji maji, utoaji umeme, nishati ya viumbe na utengenezaji wa mazao ya kilimo katika nchi nyingi za Afrika zikiwemo Guinea, Sudan ya kusini, Ethiopia, Afrika Kusini, Nigeria na Kenya. Naamini kuwa miradi hiyo itahimiza kidhahiri maendeleo ya uchumi wa Afrika na kuboresha maisha ya watu wa huko, nina hakika kampuni yetu inakaribishwa kwa dhati na watu wa Afrika." 

Zaidi ya miaka kumi iliyopita, ushirikiano ulio chini ya utaratibu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika pia umepata maendeleo makubwa. 

Ushirikiano huo umeisaidia Afrika ikuze huduma za jamii na kuinua uwezo wake wa kujiendeleza, na kuboresha maisha ya watu wa huko. 

Kuboresha huduma za matibabu ni moja ya maeneo muhimu kwa Afrika kutimiza lengo la maendeleo ya milenia la Umoja wa Mataifa, na pia ni muhimu kwa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika kuboresha maisha ya watu. 

Kuzidisha maelewano na urafiki kati ya watu wa China na Afrika ni jambo muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande hizo mbili. 

Katika upande huo, mashirika yasiyo ya kiserikali yanatoa michango mikubwa. 

Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa Tanzania waliosoma nchini China Fred Maiga alisema: 

Mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa China na Afrika ni msingi muhimu wa uhusiano mpya wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Afrika.

 Mwenyekiti wa shirikisho la Africacare la Kenya Jojo Pio alisema, anatarajia kuimarisha zaidi ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali ya China. 

"China na Kenya zimeshirikiana katika maeneo mengi, rais wa Kenya alipofanya ziara nchini China alisaini makubaliano mengi na China kuhusu ushirikiano katika sekta mbalimbali, Tukiwa wajumbe wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kenya, lengo letu ni kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali ya China na kuzisaidia serikali zitimize maendeleo ya ushirikiano katika sekta mbalimbali."


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment