Image
Image

PETER KING: ASEMA MAGAIDI WALIOVAMIA JUMBA LA KIBIASHARA NCHINI KENYA WAMEPATA MAFUNZO KATIKA NCHI YAKE.




Mjumbe wa Congress ya Marekani, Peter King amesema magaidi waliovamia jumba la kibiashara la Westgate jijini Nairobi, Kenya wamepata mafunzo katika nchi yake.

King ambaye anatoka katika chama cha upinzani cha Republicans amesema kundi hilo pia limewafunza ugaidi baadhi ya Wamarekani pamoja na Wasomali wanaoishi huko.

Huku hayo yakijiri, Marekani imesema inajipanga kushambulia vituo kadhaa vya kundi la kigaidi la al-shabab nchini Kenya.

Marekani huenda ikashambulia vituo vingine vya makundi yenye kufurutu ada barani Afrika. 

Hayo yamesemwa na kamanda wa zamani wa jeshi la Marekani, Peter Chiarelli.

Wakati huo huo, jeshi la Kenya likishirikiana na vyombo vingine vya usalama vya nchi hiyo, limeendelea na oparesheni kali ya kujaribu kuwaokoa mateka wanaoshikiliwa na wavamizi hao katika jengo la Westgate. 

Wavamizi hao wanaojumuisha raia wa kigeni kutoka nchi za Magharibi na Asia na pia raia wa Somalia walivamia jumba hilo lenye maduka mengi katika mtaa wa kifahari wa Westland siku ya Jumamosi na kuuua makumi ya watu kwa kuwapiga risasi na hadi sasa bado wanawashikilia mateka watu kadhaa ambao idadi yao bado haijajulikana. 

Waziri wa Usalama wa Taifa nchini Kenya, Joseph Ole Lenku amewaambia waandishi wa habari kuwa, serikali imedhibiti jengo zima la Westgate na kwamba magaidi wako katika sehemu moja kwenye ghorofa ya mwisho. 

Ole Lenku amewataka wanahabari kuwa makini wanaporipoti tukio hilo. 

Habari za hivi punde zinatupasha kuwa, mmoja wa magaidi amekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta akijaribu kuelekea uturuki. 

Hadi tunakwenda hewani bado oparesheni ya kujaribu kuwakamata magaidi na kuwaokoa mateka ilikuwa ikiendelea.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment