KOCHA wa zamani wa Senegal Bruno
Metsu, ambaye aliiongoza nchi hiyo kufika robo fainali ya kombe la dunia mwaka
2002, amefariki dunia akiwa na miaka 59, vyombo vya habari nchini Ufaransa
vimeripoti leo hii.
Gazeti la Local La Voix du Nord,
sports daily L'Equipe na France Football magazine wameripoti kwamba Metsu,
ambaye alistaafu kazi ya ukocha akiwa na klabu ya Al Wasl ya Dubai mwaka
uliopita ili kupambana na kansa ya utumbo, alifariki dunia usiku wa kuamkia leo
nyumbani kwake Dunkirk kaskazini mwa France.


0 comments:
Post a Comment