Nahodha
wa klabu ya Darts ya Frendz ya jijini Dar es Salaam, Hemendra Katakia
akifurahia kombe baada ya klabu yake kutwaa katika mashindano ya klabu bingwa
Tanzania yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa kuifunga klabu ya Uluguru.
KLABU ya mchezo wa Dartd ya Uluguru mkoa wa Morogoro imekubali kipigo kikali kutoka kwa klabu ya Frendz ya jijini Dar es Salaam katika mashindano ya klabu bingwa ya taifa kwa kufungwa kwa pointi 9-4 katika mchezo mkali wa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa DDC mkoani hapa.
Friendz ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo wa taifa
kufuatia kuilaza klabu ya Rose Garden kwa alama 9-5 huku Uluguru yenyewe
ikiilaza Polisi Barracks kwa ushindi wa 9-4 katika michezo yao ya nusu fainali
katika mashindano yalianza oktoba 12 mwaka huu.
Kutokana na ubingwa huo Friendz walikabidhiwa
kombe, cheti na fedha taslimu kiasi cha sh 500,000 wakati washindi wa pili
klabu ya Uluguru ikijipatia zawadi ya Kombe, cheti na fedha sh400,000.
Bingwa wa mashindano hayo atawakilisha nchi
katika mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo wa darts katika ukanda wa Afrika
Mashariki ambao mashindano hayo yatakayofanyika mwezi wan ne katika ardhi ya
nchi Kenya.
Katika mashindano hayo pia yalishirikisha
michezo ya wanawake ambapo klabu ya Kimanga ya jijini Dar es Salaam nayo
iliibuka na ubingwa wa taifa kwa upande wa wanawake kufuatia kuilaza klabu ya
Polisi kutoka jijini Mbeya huku kwa mchezaji mmoja mmoja, Irene Kihupi kutoka
klabu ya Kimanga naye akitawazwa kuwa bingwa wa taifa kumfunga mchezaji
hatari wa klabu ya Moro Queens, Fabiola Namajojo kwa pointi 5-4 katika mchezo
wa fainali.
Kwa upande wa wachezaji wawili wawili,Wambura
Msila na Pastor kutoka timu ya Uluguru walifanikiwa kunyakua ubingwa huo
kufuatia kuwabwaga, Gabriel Komba na Adelade Chikoma wa klabu ya Polisi
Barracks kwa pointi 4-1 na kujinyakulia zawadi y ash 200,0000.
Mchezaji wa Polisi Barracks, Adelade Chikoma
alitwaa ubingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kufuatia kumkung’uta
mpinzani wake, John Mlay kutoka klabu ya Kimanga kwa pointi 5-2 na kuambulia
zawadi ya sh200,000 na medali.
Mashindano ya kutafuta bingwa wa mchezo wa vishale mwaka huu
yalishirikisha mikoa sita ambayo ni Kilimanjaro,Dodoma, Morogoro,Arusha, Dar es
Salaam na Mbeya huku mashindano hayo yakishirikisha klabu 11 za wanaume na
wanawake sita.

0 comments:
Post a Comment