Redds Miss
Tanzania 2012 ambaye pia ni Miss Sinza 2012, Brigitte Alfred (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na Mkurugenzi wa Lino
International Agency, Hashim Lundenga (wa pili
kulia), Miss Tanzania wa sasa Happiness Watimanywa na Mama wa Brigitte Veridiana.
Mashingia
wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa
sherehe ya kupongeza (Brigitte) kwa kushinda nafasi ya tatu ya taji la dunia la kipingele cha urembo wenye
malengo maalum. Mrembo huyo aliwashinda warembo 127.Sherehe hiyo ilifanyika
kwenye hotel ya Giraffe Ocean mwishoni
mwa wiki.
Na Mwandishi
wetu.
Redds Miss
Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lyimo amesema kuwa ushindi wake wa nafasi ya
tatu katika kipengele cha urembo wenye malengo maalum katika mashindano ya Miss
World mwaka huu ni wa Watanzania wote.
Brigitte
alisema hayo katika hafla ya kuagwa iliyoandaliwa na waandaaji wa mashindano ya
urembo nchini, kampuni ya Lino International Agency iliyofanyika kwenye hotel
ya Giraffe.
Alisema kuwa
amefarijika sana kushinda nafasi hiyo kwani ilishirikisha warembo wote
walioshindana mwaka huu katika mashindano hayo. Alisema kuwa hakuwa kazi rahis
kushika nafasi hiyo kwani kipengele hicho ushirikisha warembo wote.
“Namshukuru
mama yangu, Verdiana Mashingia ambaye
alikuwa bega kwa began a mimi katika kuhakikisha mradi wangu wa ujenzi wa bweni
la albino wa shule ya smingi Buhangija shinyanga unafanikiwa, pongezi pia kwa
kamati ya Miss Tanzania na wadhamini, Redds,” alisema Brigitte.
“Ndoto zangu
za kuitumikia jamii hazitaishia hapa, nitaitumikia na nitaendelea kuwasaidia
Albino ambao wamenichagua kuwa barozi wao,” alisema mrembo huyo.
Aidha
Brigitte alimpongeza Hapiness na kumtaka atumie kipaji alichonacho na urembo
wake wa asili kuitoa kimasomaso Tanzania kwenye mashindano ya mwakani.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga alisema kuwa Brigitte
amefanya kitu cha kihistoria Tanzania na kuzishinda nchi kubwa mbali mbali kama
Uingereza, Ufaransa na nyingine nyingi.
Lundenga
alisema kuwa wamefarijika kwa mafanikio hayo na ndiyo maana wameamua kufanya
hafla hiyo ambayo ni ya kihistoria huku akiwapongeza wadhamini, Redds kwa
kudhamini hafla hiyo.
Alisema kuwa
ni vigumu kuamini, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa fai yao inazidi kukuwa,
tena kwa mafanikio tofauti na watu wanavyodhani.
“Mfano mzuri
ni mama yake Brigitte alivyokuwa bega kwa bega wakati wote mwanaye alivyokuwa
na taji, huu ni mfano wa kuigwa na tunaomba wazazi wafuate nyayo za mama huyu,”
alisema Lundenga.
Lundenga
alisema kuwa Brigitte ameleta changamoto kubwa kwa mrembo wa sasa Happiness
Watimanywa katika mashindano yanayofuata ya urembo ya dunia.
“Brigitte
amefanya vizuri japo hakufanikiwa kutwaa taji la dunia, kuwa namba tatu kwenye
taji la mrembo mwenye malengo ambalo kuacha taji la dunia ili linafuatia,
Brigitte anahitaji kupongezwa,” alisema.
Alisema kuwa Brigitte ameonyesha ushujaa na
kuwapita warembo kutoka mataifa makubwa dunia ambao walichuana kwenye
mashindano hayo na yeye kufanikiwa kuingia hatua ya tatu bora kwenye taji hilo.



0 comments:
Post a Comment