Image
Image

VIJANA WASKAUTI HUKO KATIVI WALIA NA VIONGOZI WANAOTAFUNA RASILIMALI ZA TAIFA LA TANZANIA.



Mmoja wa maskauti akiteremka kutoka juu ya mti wakati mafunzo ya siku nne ya maskauti wilayani mpanda wiki ya Maadhimisho ya Vijana na Kumbukumbu ya Mwalimu ya miaka 14 bila ya baba wa Taifa, mwalimu Nyerere. Lakini maskauti hao bado wanamuenzi kwa kukumbuka  kwa kukumbuka yale mazuri aliyoyaacha ikiwemo kuwa na uzalendo kwa Taifa  na moyo wa ujasiri kitu ambacho kimeanza kupotea miongoni wa mwa watanzania walio wengi hasa kizazi cha sasa.
Kamishina wa SKAUTI Jonas Clavery akiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mpanda Donald Nkoswe wakati akikagua moja ya kazi zilizofanywa na maskauti wakati wakiwa kwenye mafunzo ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao katika maeneo ya kambi baadaya ukaguzi huo wa kazi alifanya shughuli ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu hao wa  mafunzo ya awali ya skauti yaliyohusisha walimu wa shule za Msingi na Sekondari wapatao 50 mkoani humo.
..........................................................................................

Ismael Mohamed (Bin majid).

Vijana wa skauti katika mkoani wa Katavi jana  wameadhimisha siku ya  Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuenzi mambo yake aliyokuwa akiyapendelea ya uadilifu moyo wa huruma, kujituma na kuthamini uzalendo wa taifa kwa kuonesha kwa vitendo yale mambo mwalimu aliyokuwa akiyafanya na kuyapenda enzi za uhai wake sambamba na uadilifu, uzalendo.

Changamoto hiyo ilitolewa na Makamishina wa  Skauti Mkoa wa Katavi Jonas Clevery wakati akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima wakati  wa kufunga mafunzo ya awali ya Skauti   kwa walimu wapatao 50 wa Shule za Msingi na Sekondari yaliyochukua muda wa siku nne kuwafunza ukakamavu na maadili ili wakafundishe mashuleni kwao watoto maadili mema.


Katika maadhimisho hayo maskauti hao wa Mkoani Katavi wakiongozwa na Kamishina wa Skauti Mkoani humo Clavery Jonasi alieleza kuwa wameamua kuweka kambi ya maskauti nje ya Mji ili kuweza kuwapatia mafunzo ya Skauti walimu wa Shule za Msingi na Sekondari ili waweze kuelewa vizuri  umuhimu wa mafunzo ya Skauti kwa Jamii kuwa yanajenga moyo wa uzalendo kwa kuwajenga vijana hasa walioko mashuleni na vyuoni,  moyo wa ujasiri, wakizalendo wa kuipenda nchi na kuondoa migomo ya mara kwa mara inayojitokeza kwa baadhi ya  wanafunzi shuleni na vyuo hapa nchini.

Kamishina huyo alieleeza kuwa Watanzania wengi maadili yamepungua ikiwemo uzalendo tofauti na wakati wa enzi za mwalimu.

Amesema kuwa sasa hivi watu wamekuwa hawana uzalendo mawazo yao makubwa wana penda  Rushwa, uchochezi wa migomo na kupandikiza chuki isiyo na tija kwa taifa.

Kwa kuliona hilo wao kama skauti wameamua kuanzisha mafunzo ya skauti kwa walimu wa shule za msingi na sekondari  ili nao wakafundishe wanafunzi wao mashuleni kwa kuwajengea uzalendo kwa kuanza kuwafundisha kuwajengea uzalendo na kuipenda nchi kwa kuwapa mafunzo ya ukakamavu, uzalendo na ujasili hali ambayo itasaidia kuwajenga zaidi tofauti na wakati huu ambapo mambo yanaenda ndivyo sivyo.

Awali akisoma risala miongoni mwa wahitimu wa mafunzo  ya awali ya  Skauti Lucy Mzunda   alieleza kuwa miongoni mwa  changamoto  walizokabiliana  nazo katika mafunzo yao ni pamoja na ukata kwa kukosa posho ya kushiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa wao ni watumishi wa umma walimu walipashwa kulipwa posho ya siku nne kuka nje ya kituo cha kazi lakini bado hawajalipwa wanaoba kulipwa.

Changamoto nyingine ni  eneo la kuweka kambi ambalo  wameomba kukabidhiwa wamilikishwe liwe mali ya skauti ya kuwa wanaweka kambi ili waweze kulitunza na kuwa endelevu kwa ajili ya kuhifadhi mazingira yasiharibiwe kwa kuwa wao ni skauti watali tunza na kulihifadhi.

Akiongea na wahitimu wa Mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa  Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpanda Donald Nkoswe, amewataka wahitimu wazingatie yale yote waliyojifunza  na waende wakawafundishe uzalendo wanafunzi wao ili waweze kuwa wazalendo wa kupenda nchi yao

Aidha ameaahidi kushughulikia madai yao yote waliyo yatoa na kuyafanyia kazi kwa kuyafikisha katika eneo husika ili yaweze kufanyiwa kazi,katika hatua nyingine kutokana na kugushwa na mafunzo hayo ameahidi kuchangia shilingi laki moja ili kusaidia katika mafunzo ya jayo awamu nyingine ya mafunzo.

Wahitimu hao wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo, na umahili katika stadi mbalimbali za kujifunza ikiwemo ukakamavu, uadilifu,taaluma na maigizo katika mafunzo hayo ambayo yamefana  sana nakuonesha umahili wa hali ya juu kwa wahitimu waliopata mafunzo kutoka kwa wakufunzi wao.

Wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku nne yakiambata na wiki ya Vijana na maazimisho ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu NyerereChangamoto imetolewa kwa watanzania kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere  kwa  Vitendo  ili kuendana na  matendo ili kuenzi yale yote aliyokuwa akiyafanya wakati wa Utawala wake.



Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment