Image
Image

MPINGA NJIRA: JOYCE BANDA ANATISHIWA KUUAWA.




Waziri wa habari wa Malawi Bw Brown Mpinganjira amesema Rais Joyce Banda wa Malawi ambaye ametangaza vita dhidi ya ufisadi nchini Malawi amekuwa akitishiwa kuuawa. 

Vitisho dhidi ya Rais Banda vimekuja wakati maofisa wakubwa na wa kati wa Malawi wanaendelea kukamatwa kutokana na kuhusika na vitendo vya ufisadi. 

Mwezi Septemba mhasibu msaidizi wa wizara ya fedha ya Malawi alikamatwa na zaidi ya dola laki 3 za kimarekani kwenye gari yake na nyingine zikiwa nyumbani kwake. 

Mhasibu huyo alikamatwa baada ya mkurugenzi wa bajeti wa Malawi kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana, na baadaye kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu. 

Wakati serikali ya Malawi ikiendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kuuawa kwa mkurugenzi wa bajeti, kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu kamatakamata ya maofisa wa serikali wanaohusika na vitendo vya ufisadi katika serikali ya Malawi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment