Image
Image

RELI YA TANZANIA NA ZAMBIA TAZARA KULETA AHUENI SASA.




Mkurugenzi wa reli ya Tanzania na Zambia TAZARA, Bw Ronald Phiri amesema ana matumaini makubwa na uhakika kwamba reli ya TAZARA itakuwa na mustakbali mzuri hususan kutokana na vifaa sahihi pamoja na msaada wa kifedha. 

Bw Phiri amesema hayo alipokuwa akizungumza na ujumbe wa maofisa kutoka China ambao upo Tanzania kukagua miradi iliyodhaminiwa kupitia makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia kati ya China na Tanzania. 
Ameeleza kuwa amekutana na wateja wengi pamoja na makampuni ambayo yameeleza nia yao ya kuacha kutumia usafiri wa barabara na kutumia usafiri wa reli, jambo ambalo linatoa ishara ya kuwepo kwa soko kubwa kwa reli ya TAZARA. 

Kwa upande wake kiongozi wa ujumbe huo Bibi Chen Rong ambaye pia ni mkurugenzi wa divisheni ya ofisi ya utendaji ya ushirikiano wa kimataifa na kiuchumi ya wizara ya biashara ya China, amesema watu wa China wanaithamini TAZARA na kuona ni kama alama kubwa ya urafiki na ushirikiano kati ya nchi tatu za China, Tanzania na Zambia na kusisitiza kuwa China siku zote itaisaidia reli ya TAZARA.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment