Image
Image

NATO KUAGIZA VIKOSI VYA USALAMA KUIMARISHA ULINZI.




Baada ya kuwa na nafasi kuu katika kuharibu miundo mbinu ya Libya, hatimaye Muungano wa kijeshi wa (Nato) umesema kuwa utatuma timu ya wataalamu ili kuisaidia nchi hiyo ya Kiarabu kuimarisha taasisi zake za kijeshi na kiulinzi. 

Nato imesema kuwa imeafiki ombi lililotolewa na Ali Zeidan Waziri Mkuu wa Libya la kutoa ushauri katika suala la kuimarisha taasisi za kiulinzi za nchi hiyo. 

Hata hivyo nato imeongeza kuwa itaunda timu ndogo ya ushauri ya watu wasiozidi kumi kwa ajili ya kazi hiyo. 

Aidha msemaji wa NATO Carmen Roman amesema timu hiyo haitakuwa na kambi ya kudumu huko Libya na kwamba itafanya shughuli zake kutokea Ubelgiji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment