Image
Image

NYAISANGA AAGWA KWA HESHIMA ZOTE, BILALI AMZUNGUMZIA ALIKUWA MTU WANAMNA GANI, WAANDISHI NA WATU MBALI MBALI WAPATA WAKATI MGUMU WAKIMUAGA.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah Katika viwanja vya leaders Club Jijini Dar es Salaam,(Picha Na Semvua Msangi Tambarare Halisi).


 Na. Semvua Msangi,Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Billal, Amewaongoza watanzania Katika kuuga na kutoa Heshima za Mwisho  katika Msiba wa Mtangazaji  na  Mwandishi  wa Habari Julius Nyaisangah Katika Viwanja vya Leaders Jjijini Dar es Salaam.

Licha ya kuwaongoza wananchi katika kuuaga mwili huo Pia alikuwepo kiongozi wa wa kambi rasmi ya upinzani  Bungeni ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media  Regnal Mengi Sambamba na  Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania Absalum Kibabanda.

Dk Bilall alisema kuwa Kifo cha Mtangazaji huyo  wamekipokea kwa Huzuni kubwa Kama serikali kwani alikuwa ni Mtangazaji ambaye alikuwa anafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utangazaji na kuongea kitu ambacho kilikuwa kinamantiki na mashiko kwa jamii licha ya kuwa alifanya kazi kipindi ambacho viombo vya Habari vilikuwa vichache na hivyo kumpelekea ugumu katika ufanyaji wake wa kazi ,lakini wao kama serikali watamkubuka Daima kwani Kazi ya Mungu Haina Makosa na Huko ndiko Kila mja atakapo enda na kifo hakikwepeki kikubwa ni kumuombea dua afike salama Huko aendako.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema Freeman Mbowe  alisema kuwa msiba nikitu ambacho huwa kila mtu kitamkuta, nakusema kuwa wanahabari ni watu makini mno hasa katika kuandika habari zao lakini akasisitiza kuwa kuwepo wa  utamaduni wa wanahabari kuandika vitabu kwa lengo la kuwa na historia mbali mbali kwa vizazi vya sasa na vijavyo kusudi kuweza  kuwa tambua watu Maarufu na wasio Maarufu kwa kupitia Historia.

Wakati nilipo muuliza swali kwanini Wanahabari Hawana Desturi za Kuwa na utamaduni wa kuandika Historia mbali mbali katika uandishi wao, Alisema kuwa ni mfumo wa elimu wanchi yetu na endapo utarekebishwa na kukaa sawa Basi wanahabari watakuwa ni chachu ya kuandika historia kwa kuacha kumbu kumbu ya vitabu na hata vyuo vinavyo fundisha Taaluma hii ya Habari.

Naye Mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri absalum Kibanda alisema kuwa julias nyaisangah alikuwa mwalimu na kiongozi wa wanahabari, na amekuwa akiwatia hamasa  wanahabari hata walipokuwa katika shughuli zao huko mikoani, kwani nyaisangah hakuwa mbaguzi alikuwa ni mchangamfu na alikuwa mtu wa watu kwahiyo wao kama wanahabari watamkumbuka zaidi na zaidi katika taaluma hii kwani pengo lake nikubwa na hakuna wakuliziba.
Pia Meneja Matangazo wa Abood Media, Abeid dogoli akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Abood Media, Abdulazizi Mohamed Abood  alimzungumzia marehemu nyaisangah kutokana na ni mtu ambaye wamekuwa wakifanya naye kazi bega kwa bega hadi siku ya mwisho na kusema kuwa, wao kama abood media wamepata pengo kubwa kwa mtu ambaye alikuwa anaweza kuelekeza watu katika tasnia hii ya habari na mtu ambaye alikuwa  mahiri, lakini walijitahidi kwa kila namna kumuokoa maisha yake lakini kama ilivyo kuwa mungu akimuhitaji mja wake humchukua ndivyo ilivyokuwa hadi leo hii hatunaye Marehemu nyaisangah.

Hata hivyo mwenyekiti wa makampuni ya IPP MEDEDIA Regnal Mengi alisema kuwa marehemu nyaisangah ni mfano wa kuigwa kwani alikuwa mtangazaji ambaye hakuwa na majivuno mengi licha ya kuwa maarufu na mtu ambaye alikuwa kipenzi cha wengi katika sehemu zakazi, na ndio maana ataendelea kumkumbuka kwa yale aliyo yafanya na kuwataka wanahabari kuiga mfano wake, licha ya kuwa tayari wapo ambao wanafuata nyendo zake kila uchao.

Aidha Marehemu alianza elimu yake ya msingi nchini Kenya Mwanzoni mwa miaka ya 70 baada ya kumaliza alirudi nchini Tanzania na Kuanza elimu yake ya sekondari Buhemba Tarime,Alijiunga na chuo cha utangazaji nyegezi mwanza na kuhitimu mafunzo yake mwaka 1979 alirudi nchini Kenya na kujiunga na shirika la Utangazaji la Kenya  KBC wakati huo ikijulikana kama Voice of Kenya kama mtangazaji.

Sasa baada ya kufanya kazi kwa Takribani mwaka mmoja Voice of Kenya, marehemu nyaisangah alirejea nchini na kujiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) Hadi mwaka 1994 na Hatimaye kujiunga na Radio One Sterio/ ITV, alifanyakazi katika kituo hicho cha Radio one/ Itv hadi mwaka 2008  na kuhamia Radio DW ya ujerumani.

Mwaka 2010 nyaisangah alihamia Morogoro na kuanza kazi Abood Media Kama Meneja wa kituo hicho mpaka  alipofikwa na umauti tarehe 20/10/2013 katika Hospitali ya Mazimbu Mnispaa ya Morogoro. 

Marehemu nyaisangah alianza kuugua ugonjwa wa kisukari Mapema mwaka huu, Ameacha mjane Leah julius Nyaisanga,  na watoto watatu, Samweli julius nyaisangah, Noela julius nyaisanga na Beatres Julius Nyaisangah, amefariki akiwa na umri wa Miaka 53, amezaliwa 01 january 1960 huko Tarime Mara Na Maziko yatafanyika huko.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment