Image
Image

WANAMGAMBO WA BOKO HARAMU WAUAWA NA JESHI LA NIGERIA




Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wanamgambo 37 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. 

Kapteni Aliyu Danja msemaji wa jeshi la Nigeria katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi hiyo amesema kuwa jeshi lilifanya mashambulizi dhidi ya kambi ya Boko Haram huko Alagano. 

Kapteni Aliyu Danja ameongeza kuwa oparesheni hiyo iliyoanza juzi Jumatatu ilihusisha mashambulizi ya nchi kavu na angani kwa lengo la kuisambaratisha ngome ya wanamgambo wa Boko Haram huko Alagano.

 Itakumbukwa kuwa Mei 15 mwaka huu jeshi la Nigeria lilianzisha mashambulizi dhidi ya kundi la Boko Haram siku moja baada ya Rais Goodluck Jonathan kutangaza hali ya hatari kwenye majimbo matatu ya Borno, Yobe na Adamawa huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment