Image
Image

WATU KUMINATATU WAFARIKI KWA AJAJALI YA GARI SINGIDA WAKIWEMO WA FAMILIA MOJA.




WATU kumi na watatu wamefariki dunia Mkoani Singida,wakiwemo watatu wa familia moja baada ya gari aina ya Noah lenye namba za usajili Na.T730 BUX walilokuwa wakisafiria kutoka Itigi kwenda Singida kugongwa na lori lenye namba za usajili T687 aina ya AXB katika Kijiji cha Isuna,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida leo.

MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida,Dk.Deogratius Banuba amesema amepokea miili kumi na mitatu ya marehemu hao ambapo kumi na mmoja wameshatambuliwa.

Baadhi ya mashuhuda wamedai kuwa lori hilo lililokuwa likitokea Mkoani Mwanza  kwenda Dar-es-Salaam likiwa na shehena ya samaki liliacha njia na kuifuata Noah na kisha kuliparamia juu na hivyo kusababisha vifo hivyo papo hapo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, SACP,Geofrey Kamwela amesema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi wa magari yote. Kwa mara nyingine ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani.

KATIKA mwezi huu pekee wa Januari 2014, hiyo ni ajali ya pili mbaya kutokea Mkoani Singida ambayo imesababisha vifo vya watu pamoja na majeruhi katika barabara kuu itokayo Singida kwenda Dar-es-Salaam.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment