Image
Image

ZIARA YA KATAINEN MAMLAKA YA BANDARI KUSHUSHA NEEMA TANZANIA


               Waziri Mkuu wa Finland JYRKI KATAINEN

Waziri Mkuu wa Finland JYRKI KATAINEN ameishauri Mamlaka ya bandari kufanya kazi kwa kuzingatia Usalama, ubora na uharaka ili kukuza ufanisi wa bandari hiyo.

Kauli hiyo ameisema wakati alipokuwa kizungumza na watendaji wa mamlaka ya bandarai na maafisa wengine wa serikali mara baada ya kutembelea bandari ya Dar es salaam, ambapo  Bw Katainen amesema nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuiboresha bandari hiyo iwe ya kisasa.

Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na wenzao wa Finland, ulimwelezea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Finland kuwa, baadhi ya changamoto zinazoikabali mamlaka ya bandari nchini ni ukosefu wa rasailimali watu wenye ujuzi, teknolojia ya kupakia na kupakua mizigo kwenye meli pamoja na maghala ya kisasa ya kuifahidhia mizigo.

Bandari ya Dar es salaam imekuwa ikinunua baadhi ya vifaa na mitambo mikubwa ya kubebea  mizigo kutoka Finland, na pia makampuni mawili makubwa ya taifa hilo la Ulaya Kaskazini yamekuwa yakitoa huduma ya kusafirisha na kupokea mizigo yenye kemikali inayopitia bandarini hapo.

Aidha bandari ya Dar es salaam imekuwa ikipitisha mizigo inayoingia na kutoka zaidi ya tani milion 13.5 kwa mwaka. Na imekuwa ikitumiwa na mataifa jirani kwa ajili ya kupitisha mizigo yao pia.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment