Image
Image

Chanjo Mbili za Ebola zaanza kufanyiwa majaribio nchini Liberia


Chanjo za aina mbili za kukabiliana na homa ya Ebola zimeshaanza kufanyiwa majaribio kwenye hospitali moja iliyoko nchini Liberia.
Taarifa zinasema kuwa, majarib
io ya kwanza ya chanjo ya homa ya Ebola yalianza jana kwenye hospitali iliyoko nchini humo. Taarifa hizo zinasema kuwa, zoezi la kutoa chanjo hiyo linafanyika katika mradi wa 'Prevail' ambao unafanyika kwa lengo la kufanya uchunguzi wa chanjo dhidi ya Ebola nchini Liberia. Taarifa hiyo kutoka Monrovia zinasema kuwa, chanjo hizo ni ChAd3 na nyingine inajulikana kwa jina la rVSV-ZEBOV. Chanjo hizo kabla ya kutolewa kwa binadamu, ziliwahi kufanyiwa majaribio kwa wanyama.
Ofisi ya Rais wa Liberia imeeleza kuwa, chanjo hizo huenda zikaleta faraja kwa wananchi wa nchi hiyo na nchi jirani, kama vile Guinea Conakry na Sierra Leone ambazo nazo zimekumbwa na maradhi hayo.
Wakati huohuo, Wizara ya Elimu ya Liberia imeakhirisha ufunguzi wa shule nchini humo hadi 16 mwezi huu. Shule nchini Liberia zilifungwa tokea mwezi Agosti mwaka jana kutokana na kuongezeka wimbi la homa ya Ebola nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Dun
iani (WHO), zaidi ya watu 9,000 wameshafariki dunia tokea lilipoanza wimbi la homa ya Ebola na hasa katika nchi tatu za Magharibi mwa Afrika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment