Image
Image

Hali ya Jack Wilshere bado haijawa imara kurejea uwanjani

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema bado hajajua lini mchezaji wa kiungo Jack Wilshere atarejea uwanjani baada ya kujeruhiwa. 
Wilshere hajacheza tangu Novemba alipoumia kifundo cha mguu katika mechi ya Ligi Kuu ya England ambapo Arsenal ilifungwa mabao 2-1 na Manchester United. 
Kuhusu mchezaji mwingine Alexis Sanchez ambaye tayari amefunga mabao 18 msimu huu, Wenger alisema, atajiunga na kikosi kitakachocheza na Leicester na kwamba hakukuwepo majeruhi wowote katika mchezo wa Jumamosi ambapo Arsenal walishindwa na watani wao wa jadi Tottenham. 
Kwa kupoteza mechi hiyo Arsenal sasa inashiikilia nafasi ya sita katika Ligi Kuu. Mbali na Wilshere na Sanchez Arsenal pia inamkosa Alex Oxlade-Chamberlain ambaye aliumia wakati Arsenal ilipopambana na Manchester City mnamo mwezi uliopita.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment