Image
Image

JK aanza ziara ya siku mbili Lusaka Zambia



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka leo tarehe 25 Februari, 2015 kuelekea Lusaka Zambia kwa ajili ya ziara ya kikazi ya  siku mbili  kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Edgar Chagwa Lungu wa Zambia.

Viongozi hao wanatarajia kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hizi ikiwemo suala la reli ya Tanzania-Zambia Railway Authority (TAZARA),  inayounganisha Tanzania na Zambia.

Hivi karibuni Reli ya TAZARA imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitajika kujadiliwa kwa kina na viongozi wakuu ili kuimarisha zaidi reli hiyo ambayo ni kiungo kikubwa baina ya nchi hizi katika masuala ya uchumi  na alama ya ushirikiano.

TAZARA ilizinduliwa rasmi Oktoba 1975 kwa ufadhili wa China. Reli hiyo ina upana wa milimita 1,067 na urefu wa Kilometa 1, 860 kuanzia Dar es Salaam, Tanzania na kuishia katika mji wa New Kapiri Mposhi nchini Zambia.

Reli hiyo ina uwezo wa kusafirisha mizigo ya tani milioni 5 na watu milioni 3 kwa mwaka.

Rais Kikwete na ujumbe wake wanatarajiwa kurejea nchini kesho tarehe 26 Februari, 2015

……………MWISHO……………

Imetolewa na:

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,

Ikulu-DSM

25 Februari, 2015
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment