Image
Image

Breaking News:Mapya yaibuka wananchi wawasusia polisi maiti ya mama aliyefariki juzi wakati wa mapambano na Jeshi hilo ilula.


Wananchi wa Ilula wamegoma kupokea maiti ya mama aliyeuwawa wakati wa mapambano katiyao na polisi  kwa masharti kwanza kuachiliwa kwa waliokamatwa ambao badoo wanashikiliwa na polisi, pili  polisi waliouwa wakamatwe na kufikishwa  mbele ya sheria .

Mbunge wa  kilolo  Prof. Peter Msola ameshindwa kulipatia suluhu swala hilo na kuondoka eneo la tukio huku polisi wakibaki na maiti  kwenye  gari.
Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Iringa ambako mtu mmoja alifariki wakati wananchi walipopambana na polisi na baadaye kufunga barabara kwa saa tano, limeingia katika orodha ndefu ya matukio yanayozidi kuongezeka kila kona ya mapambano baina ya raia na askari wa Jeshi la Polisi.
Katika tukio la juzi, wananchi wa Ilula walimtuhumu polisi kumuua mwanamke kwa kosa la kuuza pombe muda wa kazi na hivyo kupanda ghadhabu na kuvamia kituo cha polisi ambako walichoma magari matano madogo na basi moja na baadaye kwenda kufunga Barabara ya Dar es Salaam- Mbeya kwa muda wa saa tano hadi Jeshi la Polisi lilipoongeza askari wake kutuliza ghasia hizo.

Kaimu kamanda wa polisi wa mkoani Iringa, Pudensiana Protas aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa watu 18 wamekamatwa wakihusishwa na vurugu hizo, lakini akakataa kuzungumzia mwanamke aliyekufa akisema atafanya hivyo baada ya kupokea taarifa ya daktari.
Tukio hilo ni moja tu kati ya mengi ambayo yamekuwa yakitokea katika miezi ya karibuni yakihusisha wanavijiji, walimu, wakulima, wasomi, madaktari, wanafunzi wa sekondari na makundi ya vijana ambao katika kushinikiza wanasikilizwa au kulinda haki zao, wamejikuta wakifanya vurugu zinazohusisha mapambano dhidi ya askari wa Jeshi la Polisi, uharibifu wa vyombo vya usafiri, kufunga barabara na maandamano ambayo hukatishwa kwa virungu, mabomu ya machozi na wakati mwingine silaha
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment