WAZIRI Kivuli wa
Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter
Msigwa (CHADEMA), amesema Watanzania wanahitaji rais ajaye awe na malengo,upeo
wa kutatua changamoto ili taifa liondokane na umaskini.
Mchungaji Msigwa
aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na
Kituo cha Televisheni cha ITV na kusisitiza rais ajaye lazima awe na uwezo wa
kifedha si maskini ili asiwafanye Watanzania waendelee kuwa maskini.
Alisema kama ni
tajiri, awaeleze Watanzania utajiri wake ameupata wapi isiwe umetokana na fedha
za wizi na kutaka wagombea wote wapimwe akili na uwezo wao wa kuongoza
wananchi.
"Rais ajaye awe
na uwezo wa kukabiliana na wimbi la umaskini linalowatesa Watanzania wengi,
achambue mambo na kuwapeleka Watanzania katika njia inayoleta mafanikio,"
alisema.
Aliongeza kuwa, lazima
kiongozi anayefaa kuwa rais apimwe akili na afya ili wananchi wafahamu ndipo
achaguliwe na akipita aanze kuwatumikia Watanzania akiwa na afya njema.
Aliwataka wananchi
wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika vyama vya
siasa kama ubunge, udiwani na urais ili taifa liweze kupata viongozi bora.
Mchugaji Msigwa
alisema wale wanaosema rais ajaye anapaswa kuwa kijana hicho si kigezo
kinachohitajika ili kumpata kiongozi bali awe wa umri wowote ila mwenye uwezo
wa kuchanganua mambo na mwenye dira ya kuona mbele.
Alisema Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kikiendelea kubaki madarakani mwaka huu ni majanga; hivyo
umefika wakati wa Watanzania kufanya mabadiliko.
0 comments:
Post a Comment