Image
Image

Jeshi la Polisi mkoani kagera lazima jaribio la utekaji magari katika eneo la NYAKANAZI wilayani BIHARAMULO

Jeshi la Polisi Mkoani KAGERA limefanikiwa kuzima jaribio la utekaji wa magari katika eneo la NYAKANAZI wilayani BIHARAMULO,na kukamata bunduki NNE aina ya SMG, Risasi MIA MOJA NA ISHIRINI NA TISA pamoja na sare za jeshi la nchi moja jirani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa KAGERA ACP HENRY MWAIBAMBE amesema baada ya mapambano ya kurushiana risasi na watu hao wanaosadikiwa kuwa majambazi katika pori la NYANTAKARA kwa takribani dakika KUMI, majambazi hao walitokomea mahala kusikojulikana.
Baadhi ya vitu mbalimbali vilivyonaswa na Jeshi la Polisi mkoani KAGERA ambavyo ni pamoja na bunduki NNE aina ya SMG,risasi mia moja na ishirini na tisa , MAGAZINE SITA ,pamoja na sare za nchi jirani.
Aidha katika hatua nyingine Kamanda MWAIBAMBE amewashukuru wananchi wa kijiji cha Kabale kata ya NYAMAHANGA wilayani BIHARAMULO kwa kusaidia kukamatwa kwa majambazi wawili ambao walikutwa na furushi lililokuwa na nyenzo mbalimbali zinazosaidia kutekeleza uhalifu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment