Image
Image

Makinda:Bunge lina laani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa Walemavu wa ngozi ALBINISM





Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda amesema bunge linalaani vitendo vya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Maalbino vinavyoendelea hapa nchini.

Hayo yamejiri bungeni wakati spika Makinda akitoa kauli ya bunge kuhusiana na maelezo binafsi ya mbunge wa viti maalum  ambapo pamoja na mambo mengine ameziomba mahakama kuharakisha utoaji wa hukumu wa kesi zinazohusiana na kuwajeruhi ama kuwaua maalbino.
Amesema ni jambo ambalo haliingii akilini kwa watu kudhania kuwa viungo vya wenzao vinaweza kuwapatia utajiri hivyo ni bora jamii ikapambana kutokomeza vitendo hivyo.
Awali Mhe.Shaymar  amesema hali ya maisha ya maalbino kwa sasa nchini imekuwa tete kwani wanaishi maisha ya mashaka huku wakiwa hawajui hatma ya maisha yao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment