Image
Image

Mke wa rais wa zamani wa ivory coast ahukumiwa kwenda jela kwa miaka 20

Aliyekuwa Mke wa rais wa Ivory Coast, Simone Gbagbo amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuhusika na machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Simone Gbagbo, mwenye umri wa miaka 65, alifunguliwa mashtaka ya kudharau usalama wa taifa.

Mumewe aliyekuwa rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, naye anangojea kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).

Zaidi ya watu 3,000 walikufa kwenye machafuko yaliyofuatia baada ya uchaguzi wa rais, kufuatia Gbagbo kupinga kushindwa na Alassane Ouattara.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment