Image
Image

Obama akosoa barua ya maseneta wa chama cha republican


Rais Barack Obama amekosoa barua ya maseneta wa chama cha Republican iliyotumwa kwa Iran, na kukituhumu chama hicho kwa kuingilia mazungumzo ya kusitisha urutubishaji nyuklia.

Rais Obama amesema masetena 47 waliofanya jambo hilo wameunda muungano usiowakawaida na na viongozi wa dini wenye misimamo mikali.

Barua hiyo imeikumbusha Iran kuwa makubaliano yoyote yatakayofikiwa na serikali kuu, yatakuwa na maana iwapo yataridhiwa na baraza la Congress ambalo linaongozwa na chama cha Republican.

Mazungumzo ya mpango wa kurutubisha nyuklia wa Iran upo katika hatua muhimu, huku muongozo wa makubaliano hayo ukitarajiwa kutolewa Machi 31.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment