Image
Image

Wabunge nchini kenya kuchunguza kitendo cha kenya Airways kukataa kumchukua Rais Museveni

Wabunge wa Kenya watachunguza shirika la ndege la nchi hiyo kwa kutupilia mbali ombi la kumpeleka Nairobi Rais YOWERI MUSEVENI wa Uganda.
Mbunge NDUNG'U GETHENJI amewaambia waandishi wa habari kwamba uchunguzi huo ulikuwa unahitajika kwa sababu kitendo kilichofanywa ni aibu kubwa kwa
Kenya.

Shirika la ndege la Kenya Airways lilikataa ombi la kumchukua Rais YOWERI
MUSEVENI kutoka mji wa nyumbani kwake magharibi mwa Uganda tarehe 20 ya mwezi uliopita. 

Taarifa za vyombo vya habari vya Kenya zinasema shirika hilo la ndege
limekiri kwamba tukio hilo lilikuwa la kusikitisha kwani linaharibu uhusiano
kati ya nchi hizo jirani lakini halikusema kwa nini lilikataa ombi hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment