Image
Image

Waziri Fenella azindua Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) na wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno iliyofanyika katika viwanja vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliambatana na matembezi ya hiari yalioyoanzia katika viwanja hivyo na kupitia Barabara ya Diomond Jubilee kabla ya kurudi uwanjani hapo kupitia barabara ya AlhasanMwinyi na Kauli mbiu ya wiki ya Afya ya Kinywa ni “Tabasamu la Maisha” Katikati ni Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro na wa mwisho kulia ni Rais Mteule wa Chama hicho Dkt. Ambege Mwakatobe.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akipeana mkono na Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro (kulia) jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiangalia baadhi ya machapisho yanayohusu Afya ya Kinywa na Meno kwenye banda lililowekwa katika Viwanja vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. Kushoto ni Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (wapili kutoka kushoto) akiwa katika matembezi ya amani ikiwa ni katika hfla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na wananchi wkishiriki matembezi ya amani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na wananchi wkishiriki matembezi ya amani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno jana jijini Dar es Salaam.
 Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini/WHVUM.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment