Image
Image

Waziri wa afrika kusini afa katika ajali ya barabarani na walinzi wake wawili

Waziri Collins Chabane akiwa kati kati ya Rais Zuma na kiongozi wa kike mwenye mawani.

Waziri wa Afrika Kusini Collins Chabane pamoja na maafisa wake wawili wa ulinzi wamekufa katika ajali ya gari.

Gari la waziri huyo wa Utumishi wa Umma liligongana na lori kaskazini mashariki mwa mji wa Polokwane.

Chabane, mwenye umri wa miaka 54, pia mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha ANC na rafiki wa karibu wa Rais Jacob Zuma. Pia ndiye aliyesimamia maandalizi ya maziko ya Mzee Nelson Mandela.

Rais Zuma amesema ameshtushwa mno na ajali hiyo iliyokatisha maisha ya rafiki yake na kuongeza kuwa kifo hicho ni pengo kubwa kwa serikali na taifa zima kwa ujumla.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment