Image
Image

Dk.Mengi ashtushwa na tuhuma zinazodai kuwa ana nia ya kutaka kuiangusha serikali ya Rais Kikwete.


Mwenyekiti mtendaji wa  IPP DR. REGINALD MENGI ameeleza kushtushwa na taarifa zilizochapishwa  kwenye gazeti la taifa imara  zikimtuhumu kuwa ana nia ya  kutaka  kuiangusha serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza  muda wake wa uongozi kunyamaziwa na  ikulu na idara ya habari maelezo  kwa wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote.
Katika kauli yake kwa vyombo vya habari  Dr. Mengi amesema   taarifa  ya Gazeti hilo  iliyouliza swali ,ZITTO  AMCHONGEA   MENGI KWA JK ambayo  pia  imesema Rais Kikwete  aliapa kupambana naye inampa hofu kubwa kuhusu mustakabali wa maisha yake kutokana na kuachwa kuendelea kusambaa kwa tuhuma hizo.

Amesema ukubwa wa hofu hiyo ni kutokana  na  Rais ambaye ni mkuu wa  majeshi ya ulinzi na usalama kauli yake  kama ilivyonukuliwa  na Gazeti kuwa atapambana naye  inaweza kuchukuliwa  kama agizo kwa vyombo vya dola  kumuangamiza.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment