Image
Image

Maiti 18 wametambuliwa hadi sasa kati ya 19 waliotolewa kwenye mgodi ulioporomoka na kuwafukia wachimbaji kijiji cha Karore wilayani Kahama.


Maiti  18 wametambuliwa  hadi  sasa kati  ya 19 waliotolewa kwenye mgodi  ulioporomoka na kuwafukia  wachimbaji hao usiku wa Ijumaa iliyopita.
Miili iliyotambuliwa ime chukuliwa na ndugu zao tayari kwa maziko na mwili mmoja   ambao  bado haujatambuliwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama  kwa siku  saba na baada ya hapo utazikwa na Serikali.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama,BENSON MWAMPESYA,hadi sasa hakuna miili mingine  iliyopatikana   licha ya  msaada wa mitambo ya kuchimba eneo hilo na wataalamu kutoka katika machimbo ya Bulyanhulu  ambao  tayari wameshaanza  kazi  hiyo kwa siku ya tatu leo .
Amesema  kazi inakuwa ngumu kutokana na  mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na  m ashimo  hayo  yana kina kirefu hivyo zoezi hilo linachukua muda hadi kufika katika eneo lililokuwa na wachimbaji hao chini ya ardhi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment