Image
Image

News Alert:ACT yatinga mkoani Singida kwa ziara ya sikumbili kuimarisha chama na Kufungua matawi Mkoani humo.


Timu ya viongozi  wa chama ACT wazalendo  ikiongozwa na kiongozi wao mkuu,Zitto Kabwewapo katika ziara ya siku mbili mkoani singida kwa ajili ya kukijenga na kukiimarisha chama hicho kipya.

Akizungumza mwenyekiti wa ACT wazalendo mkoani singida Wilfred Kitundu, kwenye timu hiyo yupo pia mwenyekiti wa taifa  Anna Mghwira na katibu mkuu,Samson Mwigamba.amedai kuwa maandalizi yote muhimu kwa ajili ya ziara hiyo,yamekamilika. 

Akifafanua juu ya ziara hiyo,Kitundu amesema kuwa ziara hiyoiliyoanza siku ya leo juma tano asubuhi itafungua matawi yao mapya katika kijiji cha kintiku na mawili mjini manyoni na baadaye ofisi ya kanda mjini singida.

Amesema baada ya kumaliza ziara wilayani manyoni, mchana atakwenda wilaya ya singida mjini ambapo atafungua matawi matatu ya chama hicho katika kijiji cha  kisaki, utemini, na ukombozi na  pia ofisi ya kanda.

Kitundu amesema baada ya kumalizika kwa ziara hiyo jimbo la Singida mjini,kesho yake aprili kumina sita,msafara huo  utahamia wilayani iramba  ambapo utafungua matawi ya ulemo, misigiri na sokoni kiomboi, kisha kuendelea na ziara yake mkoani shinyanga.

Mwenyekiti kitundu amewaomba wakazi wa mkoa wa Singida kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza  zitto kabwe katika maeneo atakayopita na  kuhutubia juu ya itikadi, falsafa na misingi ya chama hicho.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment