Kambi rasmi ya upinzani Bungeni
imeitaka serikali kutoa ukomo wa muda wa ambao wananchi watapatiwa vitambulisho
vya taifa na kuainisha gharama zilizotumika katika mchakato mzima wa
kutengeneza vitambulisho hivyo pamoja na kutoa taarifa ya idadi ya maghala
mapya ya kuhifadhia silaha yaliyojengwa kwa fedha zilizoidhinishwa mwaka wa
fedha uliopita ambazo ni sh bilioni 10.
Hayo yamo katika hotuba za
wasemaji wa kambi ya upinzani Bungeni wa wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga
taifa pamoja na wizara ya mambo ya ndani ya nchi wakati wa kuwasilisha
makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hizo huku baadhi ya wabunge
wakishangazwa na kitendo cha wizara ya ulinzi kupangiwa fedha na kushindwa
kuzipata.
0 comments:
Post a Comment