Image
Image

Kumezuka mapigano makali kati ya majeshi ya Kenya na wapiganaji wa kikundi cha al-Shabaab mji wa Garisa.


Kumekuwa na mapigano makali kati ya majeshi ya Kenya na wapiganaji wa kikundi cha al-Shabaab baada ya kuvamia kijiji kimoja kilomita 70 Kaskazini ya mji wa Garisa.
Wizara ya Mambo ya Ndani imesema majeshi ya usalama yalijibu mapigo kwa kukabiliana na wapiganaji hao katika kijiji cha Yumbis na kuwatimua ,  lakini hakukuwa na taarifa zozote za maafa yaliyotokea.
Mwezi uliopita wapiganaji hao wa al-Shabaab walivamia Chuo Kikuu cha Garisa na kuua watu wapatao 150 wengi wao wakiwa wanafunzi.
Katika uvamizi wa hivi karibuni inasemakana wapiganaji hao waliingia msikiti mmoja wa kijiji hicho na kuhutubia waumini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea  porini .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment