Image
Image

LOWASSA:Hatuna haja yakuwa bakuli la Ombaomba nchi ina rasilimali nyingi.


Mbunge wa Monduli Mheshimiwa EDWARD LOWASSA amesema akipewa ridhaa ya kuwa rais wa nchi hii  nguvu zake zote atazielekezea  kupambana na umaskini,kulinda rasilimali za nchi,ku boresha elimu na kuwaunganisha Watanzania .
Mheshimiwa LOWASSA aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania ametoa ahadi hiyo katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, alipotangaza nia yake ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi hiyo, kupitia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Amesema Tanzania ina rasilimali nyingi na kinachohitajika ni uongozi imara wa kutokomeza umasikini na kwamba nia yake ni kuimarisha kusimamia utekelezaji wa sera zilizo bora ili kuchochea maendeleo ya watu yatakayosimamiwa na serikali ijayo.
Aidha,amesema akipewa  nafasi hiyo ya juu nchini  atahakikisha  anadumisha muungano.anaweka misingi  imara ya kuharakisha maendeleo na,atawawezesha vijana kuondoa na tabaka la walionacho nawasionacho.
Amesema kwa vyoyote vile hiyo haiwezi kuwa kazi ya mtu mmoja ni kazi ya pamoja , hata hivyo anayeongoza timu lazima awe na mwongozo unaomuongoza.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment