Image
Image

Wakimbizi wa Burundi wamuomba Rais KIKWETE kumshinikiza NKURUNZIZA kuacha kugombea Urais.


Wakimbizi wa Burundi waliokimbilia Tanzania wamemuomba Rais JAKAYA KIKWETE na jumuiya ya kimataifa kumshinikiza Rais PIERRE NKURUNZIZA wa Burundi kuachana na dhamira yake ya kugombea awamu ya tatu ya utawala, ili kuepusha madhara zaidi yaliyosababisha waikimbie nchi hiyo.
Wakimbizi hao zaidi ya elfu hamsini wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, wametoa ombi hilo wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa MATIAS CHIKAWE katika kambi ya wakimbizi ya Nyaguru wilayani Kasulu kujionea hali halisi.
Wamesema mambo yanayoendelea nchini Burundi yako kinyume cha katiba na makubaliano ya amani yaliyofikiwa Arusha takriban miaka kumi iliyopita, hivyo wakati umefika sasa wa jumuia za kimataifa kuchukua hatua ili kusitisha uchaguzi kupisha mazungumzo ya kutafuta muafaka.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi Mheshimiwa MATHIAS CHIKAWE amewataka wawe watulivu, wafuate sheria na taratibu wakati huu ambapo jitihada za kuwahamishia kambi nyingine zikiendelea huku marais wa nchi za Afrika Mashariki wakiendelea kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment