Image
Image

News Alert:Serikali yashauriwa kuunganisha wizara katika sekta ya elimu ili kupunguza matumizi mabaya ya fedha.



Serikali imeshauriwa kuunganisha wizara zinazoshughulikia sekta ya elimu nchini ili kuondoa ama kupunguza uwepo wa mianya ya matumizi mabaya ya fedha,kuongeza uwazi katika sekta ya elimu pamoja jambo likalosaidia kupunguza matumizi makubwa ya fedha katika sekta hiyo na kuwa na bajei inayotekelezeka.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam katika mjadala uliowashirikisha wadau wa sekta ya elimu na afya nchini ambapo afisa utafiti na uchambuzi kutoka haki elimu Bwana Makumba Mwemezi amesema licha ya serikali kutenga kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya elimu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo kwa mwaka huu zaidi ya Trilioni tatu nukta mbili zinatumika katika matumizi ya kawaida badala ya kuelekezwa katika uwekezaji wa elimu.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa shirika la afya Duniani WHO Dr.Rufaro Chatora amesema ni muhimu uchambuzi ukafanyika ili kujua bajeti iliyotengwa pamoja na kuanisha matumizi yake ili kuleta ufanisi huku Bwana Robert Kasenene ambaye ni mwakilishi wa taasisi ya umoja wa mataifa hapa nchini akielezea kiwango kidogo cha fedha kilichotengwa na kuelekezwa katika sekta ya afya hususani katika suala la uzazi wa mpango.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment